Usafi ni swala linalohusu nyumbani au mwili wako pekee bali
pia ni muhimu kwa mazingira yanayotuzunguka eneo la biashara. Unapoendesha
biashara mfano chakula huku eneo ambalo unafanyia biashara likiwa limezungukwa
na maji machafu au uchafu mwingine licha ya hatari ya kuleta magojwa kwako na
kwa wateja ni rahisi sana pia kukimbiwa
na watejsa.uchafu hukaribisha nzi wanaosambaza magonjwa, kama vile kipindupindu
na magojwa mengine ya tumbo.
Kutokana na uchafu kutokuwa na faida wafanya biashara hawana
budi kuhakikisha wanatunza na kusafisha mazingira ya biashara zao kila
siku.kuna maeneo ambayo watumiaji wa
bidhaa zinazozalishwa katika mazingira machafu hawana jinsi ya kupata huduma ya
chakulahivyo kulazimika kula kilichopo katika hali yeyote.
Hakuna huruma kwa mtu mchafu Zaidi ya kumkimbia na kutafuta
eneo jingine la kulana kununua bidhaa nyingine mahali pasafi penye hewa nzuri,
mwanga wa kutosha na nafasi, ndio mteja mwenye kupenda kufahamu dhamani ya
fedha anayolipa kwa ajili ya huduma atapenda kufika kupata huduma..
Kutokana na maelezo
yanayotolewa na wataalamu wa maswala ya usafi katika biashara wakiwemo
wanaoendesha mtandao wa usafi katika biashara ni jambo la lazima.
mazingira ya kufanyia biashara yakionekana katika hali ya usafi |
Hata hivyo wanasema, baadhi ya wafanyabiashra wanachukulia
suala la usafi katika biashara kuwa jambo la hilari . inaelezwa kuwa wanafanya
hivyo wakiamini kwamba kuweka mazingira ya biashara zao kwaenye hali ni kupenda
kwa mfanya biashra husika.
Kutokana na kinachoelezwa na wataalamu katika mitandao hiyo ni
vizuri wafanyabiashara wakajiuliza, usafi ni kwa faida ya nani? Nadharia ni
kwamba hakuna anayeaweza kwenda kununua
bidhaa Fulani katika duka flani lililoko
katika eneo chafu halafu akakaa kimya.wengi huzungumza walichikiona kwa
marafiki na famialia kuonesha kuwa wamekerwa.
Kuzungumza huko kunaonyesha kukerwa , jambo ambalo kuna
mtandao unasema ndio maana wanayasema yote mabaya kwa wengine hivyo kufanya
biashara husika ishuke umaarufu na kukosa wateja .mteja mmoja akiona jambo baya
linlohusu usafi ni lazima ataifikiria afya yake.
Anapokuwa akilalamika mwingine naye anasikia na kumweleza
jirani yake.kusambaa huko kwa taarifa kunaweza kumsababishia mwenye biashara
iliyozingirwa na usafu au inayotelekezwa na wahudumu wachafu hasara.
Wafanyabiashara wanaoelewa umuhimu wa usafi wanataka wenzao
waelewe umuhimu wa usafi wanataka wenzao waelewe kuwa wateja wanao wahudumia
kwa kuwauzia bidhaa au huduma mbalimbali wanaelewa thamani na umuhimu wa usafi
wa mazingira yanayozunguka biashara.
No comments:
Post a Comment